URINARY TRACK INFECTION (UTI)

Urinary Track Infection (UTI)  ni nini ?

UTI ni ugonjwa wa maambukizi katika mfumo wa mkojo , UTI ugonjwa ambao umekuwa tatizo sugu sana hasa kwa wanawake wengi, mama wajawazito , watoto chin ya miaka mitano na wanaume japo wanaume sio sana .

UTI husababishwa na nini?

UTI husababishwa bacnateria japo kuna mambo mengine ambayo husababisha UTI kama

⚠Kutokunywa maji mengi

⚠Uchafu

⚠Kuvaa nguo za ndan za kubana

⚠kubana haja ndogo yaan unapopata haja ndogo unakaa nayo muda mrefu.

Dalili za UTI

Kupata maumivu makali hasa wakati wa  kukojoa.

Mkojo kuwa na rangi ya njano sana au rangi ya mawingu pia mkojo kuwa na harufu kali.

Kupata maumivu makali ya misuli na tumbo

kuhisi kama mkojo unakunguza pia kupata mkojo kias kidogo kila unaposikia haja ndogo .Angalizo kwa mama mjamzito ni kawaida kwa mjamzito kipindi cha mwishoni  kupata kias kiasi kidogo cha haja ndogo unapoenda haja ndongo na unakuwa unaenda mara kwa mara .

Njinsi ya kutibu UTI

✔Kunywa maji mengi kuanzia glass nane mpaka kumi kwa siku.

✔Kula mananasi, mananas yana bromelain ambayo huzuia sana UTI kula vipande vitatu had vitano kwa siku vya nanasi

✔Kunywa cranberry juice au matunda ya aina ya berry kama strawberry

✔Kula matunda ya bluberries

✔Kunywa maji weka na malimao kidogo.

✔Kunywa Mtindi kwa wingi.

✔Kula matango kwa kiwingi .

✔Kunywa vyakula na vinywaji vyenye vitamin C kama machungwa juice ya ubuyu.

✔Kunywa maji ya tangawiz kwa wingi .

✔Jitahid upate haja ndongo hasa baada ya tendo la ndoa.

✔Tumia nazi katika vyakula.

✔Meza vitunguu swaum punje tatu hasa asubuh na maji chukua swaum menya kata vipande vidogo vidogo meza na maji 🚫Angalizo usitumie kama unapressure ya kushuka vitunguu swaum kwan hushusha pressure

Pamoja na hayo yote jitahid kuvaa nguo za ndani za pure cotton 🔥Nguo za ndani zisibane sana 🔥Jisafishe na msafishe mtoto kutoka mbele kwenda nyuma na sio mbele kwenda nyuma hasa baada ya haja kubwa 🔥Usitumia chemical na sabun kujisafishia ukeni. 🔥Usibane haja ndongo

Kama unasumbuliwa fata maelekezo hapo juu pamoja na dawa ulizopewa na Dactari wako

No Comments Yet

Leave a Reply

Your email address will not be published.