UJAUZITO WAKATI UNANYONYESHA


Uzaz wa mpango ni muhim sana ili kumfanya mtoto  akue vizur pia kukusaidia hata wewe mama kuboresha afya yako. Mama unatakiwa ufikilie kubeba mimba nyingine pindi mtoto anapokuwa na miaka miwil au zaid

Inapotokea umepata mimba huku mtoto ananyonya mama endelea kunyonyesha kama hali yako ya mimba ni nzuri. Kumekuwa na iman kuwa ukiwa na mimba huku unanyonyesha utamuharibu mtoto na wengine wanasema usilale nae

Mimba haiharibu wala kuathiri ukuaji wa mtoto anayenyonya , maziwa ya mama hayasabibishi kumharisha mtoto kama wengi tunavyosikia

Joto la mama harimharibu mtoto pia, hivyo mama unapopata ujauzito huku mtoto ananyonyesha unaweza nyonyesha had miez sita ya ujauzito kama mimba haikusumbui .Ni kweli unapokuwa mjamzito kuna hormone za ujauzito ambazo huingia kwenye maziwa kwa kias kidogo ,hormone hizo hazina madhara kwa mtoto wala kwa Afya yake.

Mama unayenyonyesha huku mjamzito unatakiwa uongeze kipimo cha chakula na ule mlo kamil wenye virutubisho vyote kwan unalisha watu wawili
Mimba inapofika miez minne colostrum (maziwa ya kwanza ya mtoto huanza kutengenezwa
kuna watoto ambao huona mabadiliko ya maziwa na kuacha kunyonya wenyewe na wengine huendelea tuu

Swali ambalo kina mama wengi huniuliza ni je mtoto anaponyonya hiyo colostrum hawez malizia mwenzie akizaliwa?

Jibu ni kwamba colostrum hutengenezwa kipind chote cha mimba na huisha siku tatu had nne Mara baada ya mtoto kuzaliwa. Hivyo mtoto anayenyonya hawez maliza colostrum ya mtoto aliyetumboni

Ikiwa umepata ujauzito huku unanyonyesha na umewah kupata matatizo yafuatayo ujauzito uliopita
Muone dactar kabla ujaendelea kunyonyesha

Mimba kutoka (miscarrage).

kukatazwa kufanya mapenz kipind unaujauzito.

unamimba ya mapacha.

Mtoto aliyetangulia ulimzaa premature.

Bleeding kipind cha mimba iliyopita.

1 Comment
  1. Nimeelewa vyema ila miscsrage niliipata mimba ya kwanza ya pili nikajifungua na hii ni ys tatu iliyonikuta nanyonyesha so haina tatizo?na pia sijui kama ni pacha au single maana ina week 5 tu

Leave a Reply

Your email address will not be published.