TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU(ANEMIA) KWA MAMA MJAMZITO

 Upungufu wa damu husababishwa na nini?

Upungufiu wa damu husababishwa na ukosefu wa madni chuma mwilini (Iron). Mwili unaitaji madini chuma kwa wingi kwa ajili ya kutengeneza chembe hai nyekundu  za damu (red blood cell)

Je ni kweli ninapokuwa mjamzito damu yangu hupungua?

 Ndio unapokuwa mjamzito  kiwngo cha madini chuma (Iron) yanayotakiwa mwilini huongezeka kutoka 18 milligram kwa siku mpaka 27 milligram kwa siku hii ni kutokana na mwili kuhitaji damu nying kwa ajili ya kufanya kaz mbalimbali zinazoongezeka mwilini kwa ajili ya kusapoti ukuaji wa mtoto.

Damu ni muhimu sana kwa mama mjamzito. Hivyo basi jitahid kula vyakula vyenye kuongeza Damu.

Vyakula vinavyoongeza Damu vimegawika katika makund mawil 👉Heme Iron hivi ni vyakula ambavyo mwili huweza kuichukua kirahis Iron yake navyo ni

Nyama ,Samaki,  Kuku, Maini na Dagaa

Pia kuna Non Heme hivi ni vyakula ambavyo vina Iron ya kutosha ila mwil hauwez kuichukua kirahis hivyo bas unapokula vyakula hiv jitahid kula na vyakula vyenye vitamin C kama Machungwa mapapai Nyanya na hoho
ili usaidie kuchukuliwa kwake.

Mfano wa vyakula hivi ni  Beetroot ,Mboga zamajani zote hasa matembele na spinach.

Juice ya  tembele na passion husaidia kuongeza damu kwa haraka hasa kwa wale ambao beetroot imewashinda , hii juice inaongeza damu kwa haraka sana .

Njins ya kuandaa

Oha matembele yako kwenye maji ya vuguvugu kuondoa uchafu ukimaliza yakate Kate weka kwa blender na mbengu za passion saga na maji, ukimaliza chuja juice yako japo unaweza kunywa hivyo hivyo au ukaongezea sukari.

Unaweza changanya na ubuyu mweupe pia badala ya passion .Ubuyu mweupe utatumia juice yake
Kunywa Mara mbil kwa siku kadri uezavyo ladha yake ni nzur huwez shidwa tumia .
Vyakula vingine ni ✔Mayai mayai ya kienyeji ✔Greenbeans.
✔Maboga
✔Tambi
✔Viaz vitamu
✔Tende unaweza changanya na maziwa fresh ✔Viaz mbatataau viaz ulaya ✔Maharage
✔viaz vitamu
✔njegere ✔ndegu
✔Karanga ✔almond
Mbengu za maboga
Kunde chemsha kunywa maji yake au supu yake.
Majani ya parachichi ,chemsha kunywa maji yake
Unapokula vyakula vyenye Iron usinywe na chai , kahawa au soya   huzuia( absorbtion) kuchukuliwa kwa madini chuma ( Iron)
Pia unapokunywa vidonge vile vya Damu ulivyopewa clinic baada ya kumeza unatakiwa ule na Chungwa au Papai viweze kuchukuliwa mwiln kirahis.

Dalili za kupungukiwa damu kwa mama mjamzito

Mama mjamzito unapohisi dalili  zifuatazo ni vizuri kupima wing wa damu , kwani kiasi cha damu kinatakiwa kisiwe chini ya 11g/dL mpaka mama unapoenda kujifungua

Kuchoka sana, japo kuchoka sana ni hali ya kawaida kwa mama mjamzito , hivyo unapoona unachoka sana ni vizur kwenda kuangalia wingi wa damu.

kukosa pumzi (breathless)

Kizunguzungu

Maumivu makali ya kichwa

Miguu kuishiwa nguvu

Midomo kupauka

kupata hamu ya kula udongo, ice (mabarafu ) na vitu vyote ambavyo sio vyakula.

 

Angalizo , mama jitahidi kiwangu cha damu yako kiwe 11g/dL na kuendelea kipindi chote cha ujauzito kwani upungufu wa damu unaweza kusababishwa mtoto akazaliwa na uzito mdogo, kuzaliwa kabla ya muda

No Comments Yet

Leave a Reply

Your email address will not be published.