RHESUS FACTOR (RH) KWA MAMA MJAMZITO

 

 

Leo tuangalia kidogo umuhumu wa mama mjamzito na baba  mjamzito  kujua RH group yao .

Mama mjamzito unapoenda klinik ya kwanza Mara nying mama huchukulia vipimo vya damu Vingi. Mojawapo ya kipimo ni kujua group lako la damu kama ni A,B,AB au O pamoja na rhesus factor yako kama ni( +au – )negative au positive.

Watu wengi sana ni Rh positive yaan unakuwa A ,AB,B,O+. Na wachache ni negative .

Shida inakuja pale mama anapokuwa ana rhesus negative halafu abebe mtoto mwenye rhesus positive au Mme anapokuwa positive+. Kwa mama mwenye rhesus positive hana shida yeyote  kuhusu azae na mwanamme mwenye group lipi kwani unapokuwa rhesus positive tayari unakuwa na( D protein) kwenye damu yako.


Mama mjamzito unapokuwa unablood group ambayo ni negative hakikisha unajua na mmeo group yake kama ni positive au negative  mara baada ya kupata ujauzito.
Kwani mmeo anapokuwa positive na wewe negative ni rahis kuwakinga watoto hasa mtoto wa pili na watoto wanaofuata.  Kwani tatizo mara nying huanzia kwa mtoto wa pili kama mama hakuchoma sindano kwa mtoto wa kwanza za Anti -D ambazo zitasaidia mwilini kuzuia antibodies zisitengenezwe mwilini kwa ajil ya kumdhuru mtoto hasa unapopata mtoto ambae ni rhesus positive.
Hivyo mama unapojigundua kuwa ni rhesus negative- na mmeo ni positive+ ni vizur kumueleza dactar wako mapema.

Madhara ya mama mwenye rhesus negative anapozaa mtoto mwenye rhesus positive ni pamoja na mtoto kuzaliwa na tatizo la upungufu wa damu(Anemic)

Ini kushidwa kufanya kaz vizur na kusabisha manjano,
Matatizo ya moyo kwa mtoto Angalizo sio kila manjano inasababishwa na rhesus factor .

Mama mwenye blood group positive haitaji sindano za Anti -D hata kama mmeo atakuwa ana blood negative au positive. Kwani unapokuwa positive+ unakuwa na protein D antigen ndani ya mwili wako
Share na rafiki asome.

 

 

No Comments Yet

Leave a Reply

Your email address will not be published.