TATIZO LA KUSHIDWA KUPUMUA KIPINDI CHA UJAUZITO

TATIZO LA KUSHIDWA KUPUMUA VIZURI KIPIND CHA UJAUZITO (BREATHLESS)

Tatizo la kushidwa kupumua ni tatizo linalowapata baadhi ya wajawazito. Hii wakati mwingine husababishwa na mtoto kukua na kukandamiza mbavu za mama .Tatizo hili linaweza anza mwanzon wa mimba katikat au mwishoni

Baadhi ya vitu ambavyo hupelekea mama kushidwa kupumua ni kama:
Mama kuongezeka uzito, kuwa na uzito  mkubwa .
Mama mwenye mapacha pia anaweza pata hali hii ya kushidwa kupumua.
Mwenye tatizo la kifua (asthma) kabla ya ujauzito.
Anemia mama ukiwa na damu ndogo wakati mwingine hupelekea kushidwa kupumua kwani mwili unashidwa kutengeneza red blood cell ambazo husafirisha oxygen sehem mbalimbali za mwili. Hivyo unapokuwa na tatizo la kushidwa kupumua ni vizur kucheck damu pia

DALILI ZA HATARI ZINAZOAMBATANA NA KUKOSA PUMZI

Kushidwa kupumua kunakoambatana na mapingo ya moyo kwenda mbio.

Kushidwa kupumua kunakoambatana na maumivu ya kifua.

Kushidwa kupumua kunakombatana na kuzimia.

kushidwa kupumua unapolala.

Mama ukiona hiz dalili ni vizuri kwenda kituo cha Afya

MAMBO YANAYOSAIDIA MAMA APUMUE VIZURI

mama jitahid kufanya mazoez hasa ya kutembea au kuogelea( swimming)

Kunywa maji walau lita mbil  hadi tano kwa siku.

Punguza unywaji wa chai yenye majani kahawa soda

Kula mlo kamil

No Comments Yet

Leave a Reply

Your email address will not be published.